Ummy: Tuzingatie ushauri kabla ya kutumia dawa
Dar es Salaam. Serikali imeeleza kuwa matumizi yasiyo sahihi ya dawa ndiyo chanzo cha usugu wa vimelea dhidi ya dawa (Uvida). Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alipokuwa akizungumzia kampeni inayoendelea nchini ya kukabiliana na Uvida, iliyopewa jina ‘Holela-Holela itakukosti’. Kampeni hiyo ilizinduliwa jijini hapa mwishoni mwa Mei mwaka huu kwa uratibu wa…