HISIA ZANGU: Kwa Fredy Michael utachukua namba au unachokiona?
FREDY Michael, rafiki yangu Ahmed Ally wakati akijitamba na vifaa ambavyo vilitua Januari alimpachika jina la ‘Fungafunga’. Wakati huo tulikuwa hatujamuona uwanjani. Jina lilitokea mazoezini. Kama sio mazoezini basi alikuwa amelichukua kutokana na mabao aliyofunga Zambia. Baada ya hapo Fredy ametuchanganya akili. Kila tulipomuona uwanjani alituchanganya akili. Mpaka nyakati hizi nikiwasikiliza Wanasimba wenyewe wanajikuta wamechanganyikiwa…