BILIONI 136.2 ZIMETUMIKA UREJESHAJI WA MIUNDOMBINU BARABARA NA MADARAJA
Serikali imetoa jumla ya Shilingi Bilioni 136.2 kupitia Wakala ya Barabara (TANROADS) na Wakala ya Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA), kwa ajili ya kurejesha hali ya awali ya miundombinu ya barabara na madaraja yaliyoharibiwa kwa kiasi kikubwa na janga la mvua za El Nino. Hayo yameelezwa na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba Bungeni…