Mmiliki wa duka mbaroni akidaiwa kumlawiti mtoto wa miaka 14

Iringa. Jeshi la Polisi mkoani Iringa  linamshikilia mmiliki wa duka, Blass Nicholous (35) maarufu  Matowa mkazi wa Mtaa wa Kitasengwa, Kata ya Isakalilo Manispa Iringa  kwa tuhuma za kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka 14. Mfanyabiashara huyo anatuhumiwa kumlawiti  mtoto huyo ambaye ni mhitimu wa darasa la saba mwaka jana, baada ya kumpa  kazi ya…

Read More

Viongozi wa nchi za G7 wakubaliana kuipa msaada Ukraine – DW – 13.06.2024

Kwa mwaka wa pili mfulilizo, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy atahudhuria mkutano huo, akishiriki katika mazungumzo hayo leo Alhamisi. Rais Zelensky amesema anatarajia “maamuzi muhimu” katika mkutano huo ambapo pia atatia saini makubaliano ya usalama na Japan na Marekani. Viongozi wa G7 wanatarajia kutangaza angalau kimsingi mpango wa kuipa Ukraine mkopo wa dola bilioni 50 …

Read More

Aliyehukumiwa kifungo miaka 30 jela kwa unyang’anyi aachiwa huru

Arusha. Mahakama ya Rufani Tanzania  imemwachia huru, Grace Omary aliyekuwa akitumikia kifungo cha miaka 30 jela alichohukumiwa kwa kosa la kumpora mwanamke mwenzake fedha taslimu Sh300,000 kwa kutumia silaha baada ya kushinda rufaa yake. Grace ambaye alijiwakilisha mwenyewe kortini, alihukumiwa kifungo hicho na Mahakama ya Wilaya ya Tarime, akakata rufaa Mahakama Kuu lakini akakwaa kisiki…

Read More

Waagizaji wa mafuta nchin waondolewa hofu juu ya ukarabati wa boya la kushushia mafuta ya nishati aina ya dizel

Mkurugenzi wa bandari ya Dar es salaam , Mrisho mrisho amewaondoa hofu waagizaji wa mafuta nchini kuwa ukarabati utakaofanyika katika boya la kushushia mafuta ya nishati aina ya dizel baharini kupitia bomba la tazama hautakuwa na athari katika ushushaji wa mafuta. Ameyasema hayo jijini Dar es salaam baada ya kutembelea eneo la kushusha mafuta ya…

Read More

NBC KUIMARISHA USHIRIKIANO NA WATEJA MKOANI DODOMA .

Benki ya Taifa ya Biashara kupitia timu ya kitengo cha Biashara na Uwekezaji (CIB), imefanya Ziara ya kukuza ushirikiano pamoja na ubunifu kwa wateja katika tasnia ya Benki Mkoani Dodoma. Aidha katika ziara hii Timu ya NBC ilipata nafasi ya kumsalimu Mhasibu Mkuu wa Serikali Ndg.Leonard Mkude katika Ofisi za Wizara ya Fedha Dodoma pamoja…

Read More

AKILI ZA KIJIWENI: Simba, Mo Dewji wayamalize kiungwana

SIMBA na Mohammed Dewji hakuna anayepaswa kumnyooshea kidole mwenzake katika hili linaloendelea hivyo jambo la msingi lazima wakae chini wayamalize. Kila upande umefanya makosa ambayo kwa kiasi kikubwa yamechangia kuvuruga hali ya mambo ndani ya klabu hiyo leo hii hadi kufikia hatua ya watu kusutana hadharani. Klabu kwa upande wake imeshindwa kukamilisha mambo muhimu yanayohitajika…

Read More

TANESCO KUUNGANISHA MKOA WA KAGERA KWENYE GRIDI YA TAIFA

*Mkakati kwa mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha Umeme Benaco -Kyaka wa Kilovoti 220 kuanza Desemba Na Chalila Kibuda,Michuzi TV Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema kuwa mkakati waliouweka katika Mkoa wa Kagera ni kuondokana na ununuzi wa Umeme nchini Uganda. Ununuzi wa Umeme kutoka nchini Uganda ni Megawati 21 kwa mwezi ambapo Shirika…

Read More

Asilimia 41 ya maji yaliyopimwa mwaka 2023 hayana viwango

Dar es Salaam. Asilimia 41.6 ya sampuli 5,764 za maji kwa ajili ya matumizi ya majumbani zilizofanyiwa vipimo mwaka 2023 zilikuwa hazikidhi viwango vya ubora na usalama wa maji vinavyokubalika kimataifa. Hayo yamebainishwa kupitia Kitabu cha Hali ya Uchumi wa Taifa kilichotolewa leo Juni 13, 2024 bungeni jijini Dodoma. Kitabu hicho kinaeleza kuwa, katika mwaka…

Read More