TUNAWASAIDIA WAWEKEZAJI WAZAWA KUWA MAHIRI-WAZIRI MKUU
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kuwajengea uwezo Watanzania wanaojishughulisha na masuala ya uwekezaji na kuweka mazingira wezeshi ili kuwasaidia wawe mahiri. Amesema kuwa sera za uwekezaji nchini zinatoa unafuu kwa watanzania kuingia kwenye uwekezaji na Serikali itaendelea kufanya maboresho ili wapate nafasi ya kuwekeza. Amesema hayo leo Alhamisi (Juni 13, 2024) wakati akijibu…