Kagera kuachana na umeme wa Uganda, Sh30 bilioni kuokolewa
Dar es Salaam. Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema kiasi cha Sh2.6 bilioni zitaokolewa kwa mwezi ambazo ni zaidi ya Sh30 bilioni kwa mwaka zinazotumiwa kununua umeme nchini Uganda unaotumika mkoani Kagera. Hatua ya kuokoa fedha hizo imekuja kufuatia Tanesco kusaini mkataba na Mhandisi mshauri kutoka nchini Misri (Shaker Consultancy Group) atakayesimamia ujenzi wa mradi…