THBUB YAKUTANA NA KATIBU TAWALA TABORA

Leo Juni 12, 2024 Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imekutana na Kufanya mazungumzo na Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Dkt John Mboya. Ujumbe wa THBUB uliongozwa na Mhe.Mohamed Khamis Hamad, Makamu Mwenyekiti wa THBUB. Katika ziara hiyo Mhe. Mohamed aliambatana na Mkurugenzi Msaidizi na Maafisa wa THBUB. Mhe.Mohamed alieleza kuwa lengo…

Read More

Ujenzi wa vyuo vya ufundi kuanza Ushetu

Serikali imesema kuwa kuanzia mwaka wa fedha 2024/2025 imeadhimia kujenga vyuo vya fundi katika majimbo na maeneo yote ambayo hakuna Vyuo vya ufundi na Veta. Akiongea bungeni jijini Dodoma Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mh.Omary Kipinga wakati akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani alilouliza “ni lini Serikali itaanza ujenzi…

Read More

Ziara ya Dk Nchimbi mikoani na maagizo kwa mawaziri 11

Ziara ya wajumbe wa Sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi (CCM) katika mikoa mitano imewaweka mtegoni mawaziri 11 wanaopaswa kutekeleza kero za wananchi na maelelezo ya viongozi hao wa chama tawala. Wajumbe hao wakiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Dk Emmanuel Nchimbi wamefanya ziara mikoa ya Singida, Manyara, Kilimanjaro, Arusha na Tanga kuanzia Mei 29 na…

Read More

Wabunge waibana Serikali madeni ya bilioni 285 kwa watumishi

WABUNGE wameita Serikali kuanza kulipa riba ya madeni watumishi wa umma yanayohusu likizo, uhamisho, na kusafirisha mizigo baada ya kustaafu kama inavyofanya kwa wakandarasi ambao wanacheleweshewa malipo yao. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea). Pia wameitaka Serikali kuzingatia muongozo wa 2009 wa kanuni za utumishi wa umma unaohusu udhibiti wa ongezeko la madeni ya serikali kwa…

Read More

Tanesco Kagera kuwachukulia hatua vishoka, makandarasi wasio na leseni

Kagera. Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) mkoani hapa limejipanga kuwachukulia hatua kali makandarasi wadogo wasio na leseni na mafundi vishoka wanaovaa sare zenye nembo ya shirika hilo kuwatapeli pesa wananchi. Vishoka hao wamekuwa wakiwatapeli wananchi  kwa ahadi ya kuwaunganisha na huduma za umeme. Hayo yamebainishwa katika kikao kazi kilichofanyika Juni 11, 2024 baina ya Meneja…

Read More

Serikali yamaliza mgogoro wa ardhi wa muda mrefu

Dodoma. Serikali ya Tanzania imemaliza mgogoro wa muda mrefu wa ardhi kati ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa), Kitulo,  Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) na wananchi wa kata za Ilungu, Igoma na Inyala. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Dustan Kitandula ameyasema hayo leo Juni 12, 2024 wakati akijibu swali la msingi…

Read More

Mahitaji ya umeme yamefikia asilimia 15 kwa mwaka

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko mahitaji ya umeme Tanzania yameongezeka kutoka asilimia 10 hadi 15 kwa mwaka kutokana na kuongeza kwa mahitaji, wateja na shughuli za kiuchumi. Amesema ongezeko hilo pia limetokana kuongezeka kwa vyanzo vya umeme vinavyotegemewa ambavyo ni maji yanayochangia asilimia 39, gesi asılıa inayochangia asilimia 56.1, mafuta…

Read More