Babi: Hawa kina Saido, Pacome freshi tu
NI kweli siku hazigandi, lakini rekodi ya Abdi Kassim ‘Babi’ a.k.a Ballack wa Unguja inaendelea kuishi katika vichwa vya mashabiki wa soka nchini. Ndio. Fundi huyo wa mpira aliyekuwa mahiri kwa kufumua mashuti makali uwanjani akiwatungua makipa, anaendelea kukumbukwa kutokana na rekodi aliyoiweka ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa…