Dk Nchimbi ataka kibano kwa watumishi wazembe
Moshi. Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi ameitaka Serikali kuendelea kupambana na kuwachukulia hatua watumishi wa umma wanaotanguliza maslahi yao binafsi badala ya wananchi. Dk Nchimbi amesema kila mmoja kwenye eneo lake anapaswa kula kiapo cha uaminifu cha kuitumikia nchi kwa uzalendo na hivyo kuchochea maendeleo kwa Taifa. Dk Nchimbi amesema…