Benki ya Korea yaipa Serikali mkopo Sh427 bilioni ujenzi wa hospitali Zanzibar
Seoul. Serikali ya Tanzania imepokea mkopo wa Dola za Marekani 163.6 milioni (Sh427.8 bilioni) kutoka Benki ya Exim ya Korea, kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Binguni Zanzibar pamoja na kituo cha mafunzo ya utabibu. Mkataba wa mkopo huo umesainiwa leo Jumatano Juni 5, 2024 kati ya Katibu Mkuu wa…