Mhasibu Jiji la Mwanza afariki ajalini akienda kwenye mazishi
Mwanza. Mhasibu wa Idara ya Mapato ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Amon Joseph (41) amefariki dunia katika ajali ya gari akienda kwenye maziko ya baba mzazi wa mhasibu mwenzake, yaliyotarajiwa kufanyika leo wilayani Kwimba mkoani hapa. Akizungumza na Mwananchi kwa simu leo Jumanne Juni 4, 2024, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa…