Serikali kuzindua sera ya Taifa Uchumi wa Buluu
Na Nora Damian, Mtanzania Digital Sera ya Taifa ya Uchumi wa Buluu inatarajiwa kuzinduliwa rasmi Juni 5, mwaka huu wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yatakayofanyika kitaifa jijini Dodoma. Sera hiyo ya mwaka 2024 inalenga kuimarisha mfumo jumuishi wa uratibu miongoni mwa wadau wanaosimamia na kutekeleza shughuli za Uchumi wa Buluu…