Makonda: Nitawapiga spana wazembe mpaka wanyooke
Arusha. Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesema hatishiki na kauli zinazotolewa na baadhi watu wanaomkosoa na kuwa atawapiga ‘spana’ (atawasema) wazembe hadi wanyooke. Amesema kauli hizo za wakosoaji zinamsaidia kufanya kazi kwa morali kubwa zaidi. Makonda ametoa kauli hiyo zikiwa zimepita siku nne tangu alipodaiwa kumdhalilisha mhandishi wa kike katika halmashuri ya Longido…