Maafisa watatu waandamizi wa Syria wahukumiwa Ufaransa – DW – 25.05.2024
Maafisa hao ni wa ngazi za juu zaidi nchini Syria kushitakiwa kwa uhalifu dhidi ya ubinaadamu katika mahakama ya Ulaya. Mashitaka dhidi yao yalihusisha kisa cha kupotea kwa raia wenye uraia pacha wa Syria na Ufaransa ambao ni Mazzen Dabbagh pamoja na mwanae Patrick waliokamatwa na maafisa hao, na baadae waliripotiwa kufariki wakiwa korokoroni. Rais…