FYATU MFYATUZI: Namna ya kuukwamua mgongano-muungano wetu
Fyatu Mfyatuzi, mwanazuoni, mzalendo, na mwanamapinduzi asiye kifani, nimejitoa kuchangia madini ya kuondokana na mgongano-muungano. Sihitaji kukaribishwa wala kulipwa kusaidia kufanikisha azma ya kuwa na kaya tulivu yenye mshikamano ambavyo haviwezi kupatikana kwa kuogopana, kudanganyana, kuzidiana akili au kufyatuana ilivyo. Muungano unataka vichwa vinavyochemka, ukweli, ushupavu, uwazi, uzalendo na utayari kufanya ambacho kimombo huitwa ‘give…