PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO MEI 21,2024
Home » PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO MEI 21,2024 Featured • Magazeti About the author
Home » PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO MEI 21,2024 Featured • Magazeti About the author
Dodoma. Mwili wa Askofu Mkuu wa Makanisa ya Methodist Tanzania (TMC), Askofu Joseph Bundala (55) amezikwa kwenye kanisa la Methodist lililopo Ihumwa jijini Dodoma bila kupewa heshima za mazishi kama kiongozi mkuu wa kanisa hilo kutokana na kujinyonga hadi kufa kitendo, ambacho kanisa hilo linaamini ni dhambi. Mazishi hayo yamefanyika leo Jumatatu, Mei 20, 2024…
Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa Maagizo 10 kwa Wizara ikiwemo Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Fedha,Wizara ya Kilimo,Ofisi ya Raisi Tamisemi,Wizara ya mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Vyuo vya mafunzo ya nyuki ikiwemo chuo cha kilimo SUA,Wananchi na Vyombo vya…
Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetabiri kimbunga “Ialy” kinapungua nguvu yake huku kikielekea kaskazini, mbali na pwani ya Tanzania. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo jioni Jumatatu, Mei 20, 2024 na TMA kuonesha mwenendo wake imesema kimbunga hicho kinatarajiwa kuisha nguvu yake kabisa usiku wa kuamkia keshokutwa Jumatano, Mei 22,…
Na John Mapepele. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango ametoa maelekezo kumi yatasaidia kuimarisha sekta ya nyuki ili iweze kuchangia mapato ya Serikali na kwenye uchumi wa taifa kwa ujumla. Mhe. Mpango ametoa maelekezo hayo leo Mei 20,2024 kwa wadau mbalimbali wa sekta hiyo kwenye kilele cha…
Dodoma. Serikali imewaondoa hofu Watanzania kuwa Soko la Afrika Mashariki lilopo katika Jengo la China Plaza, Ubungo jijini, Dar es Salaam halitaua soko la Kariakoo. Hayo yamesemwa leo Jumatatu Mei 20, 2023 na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Ashatu Kijaji wakati wa semina ya wabunge katika ukumbi wa Pius Msekwa. Semina hiyo ilihusisha taasisi…
NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeungana na mataifa mengine duniani kufanya maadhimisho ya siku ya Vipimo ambayo hufanyika Mei 20 kila mwaka ambapo TBS imeitumia maadhimisho hayo kutoa elimu na hamasa kwa wadau wa vipimo kuhakiki vipimo kwa lengo la kumlinda mtumiaji. Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 20,2024…
MASHABIKI wa Yanga kwa sasa wana raha mara mbilimbili, mojawapo ikiwa ni kutokana na kufanya vizuri kwa timu yao na pili mchakato wa kuboresha kikosi chao umeanza kwa ajili ya msimu ujao. Rais wa Yanga, Hersi Said ameonakana DR Congo kwa ajili ya kumalizana na baadhi ya wachezaji ambao kocha wa timu hiyo, Miguel Gamondi…
Morogoro. Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro linamshikilia Paschal Elias (18) kwa tuhuma za kutaka kuwauwa ndugu zake watatu baada ya kuwamwagia kimiminika kinachodhaniwa kuwa cha mlipuko na kuwasababishia majeraha makubwa ikiwemo yeye mwenyewe. Akizungumza na Mwananchi Digital leo Mei 20, 2024, Kamanda wa jeshi hilo mkoani Morogoro, Alex Mkama amesema tukio hilo lilitokea Mei…
NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV BENKI ya Equity imezindua Dirisha la Wanawake – Mwanamke Plus ambalo ni mpango maalum unaolenga kuwainua wanawake katika sekta ya biashara na uchumi ambapo natoa fursa za kipekee za mikopo, bima, mafunzo ya biashara, na huduma za ushauri, ikiwemo uwezeshaji wa kidigitali kupitia Equity Mobile na huduma za kibenki mtandaoni….