Mfanyabiashara awaumbua watumishi Arusha, Takukuru waanza kuwahoji
Arusha. Tuhuma za kughushi nyaraka, uchepushaji wa makusanyo ya Serikali na ubadhirifu wa fedha za umma, zimekiweka shakani kibarua watendaji wa Jiji la Arusha wakiongozwa na Juma Hamsini. Mashaka hayo, yanatokana na amri ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda kwa Katibu Tawala wa mkoa huo, Missaile Mussa awasimamishe kazi watumishi hao kupisha uchunguzi…