Mwamba wenye sura za binadamu wageuka kivutio Same
Same. Unaweza kuwa ni moja ya miamba ya aina yake kuwahi kuonekana nchini Tanzania unaopatikana katika Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, unaoonekana kama taswira ya binadamu. Pamoja na mwamba huo wenye taswira ya mwanaume, pembeni yake, kushoto na kulia, zipo taswira mbili za wanawake wanaoonekana ni wajauzito. Yohana Ramadhani (70), mkazi wa Kijiji cha Kambeni,…