
JICHO LA MWEWE: Chasambi anakitu mguuni, amahitaji kuwa ‘kiburi’
ALHAMISI nilikwenda uwanjani kutazama mechi ya Simba na Azam. Simba na Azam? hapana. Ni Azam na Simba. Azam walikuwa nyumbani siku hiyo. Siku hizi mechi zao kubwa huwa wanacheza katika uwanja wa taifa hata kama wapo nyumbani. Nilikutana na winga wa Simba anayeitwa Ladack Chasambi. Naambiwa Simba walilipa pesa nyingi kupata huduma za kinda huyu…