
PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO MEI 12,2024
Home » PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO MEI 12,2024 Featured • Magazeti About the author
Home » PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO MEI 12,2024 Featured • Magazeti About the author
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam May 12, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma za Magazeti ya Tanzania. The post Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo May 12, 2024 first appeared on Millard Ayo.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema michezo ni zaidi ya afya na burudani, ni fursa ya ajira na pia hupunguza magonjwa mwilini. “Kama mnavyofahamu, michezo ni zaidi ya afya na burudani lakini leo tunathibitisha kuwa baada ya mbio hizi, sote tumefurahi na miili yetu imeimarika.” Ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Mei 11, 2024) wakati akizungumza na…
Waziri wa Viwanda na Biashara,Mhe Dkt. Ashatu Kijaji amesema Serikali inaendelea na mchakato wa kuandaa mfumo mmoja wa ukusanyaji wa kodi kwa wafanyabiashara nchini ili kuondoa kero ya taasisi mbalimbali za Serikali kukusanya kodi. Alitoa kauli hiyo Mei 10, 2024 jijini Mbeya wakati wa Mkutano wa Majadiliano kati ya Sekta umma na Sekta binafsi uliokuwa…
Unguja. Wakati sekta ya ujenzi ikitajwa kuwa miongoni mwa zinazochangia kwa kiasi kikubwa kuharibu mazingira, wahandisi wameshauriwa kujifunza matumizi ya teknolojia ya chuma ambayo ni rahisi na rafiki kwa mazingira. Pia, wataalamu hao wametakiwa kuzingatia maeneo ya urithi wa dunia wanapoendesha shughuli zao ili yaendelee kuwa katika sura ileile. Hayo yalibainika jana, wakati wa mkutano…
Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati-Rais Samia atunukiwa Tuzo ya Ubinadamu; -Ombi la ruzuku kwa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania lafanyiwa kazi; Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa Serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania (Tanzania Redcross Society) katika utoaji…
Morogoro. Kutokana na uhaba wa viti, meza na madarasa, wanafunzi wa sanaa katika Shule ya Sekondari Ifakara wilayani Kilombero, wanalazimika kutumia maabara kusoma masomo yasiyohusiana na sayansi. Wanafunzi hao ni wale walio katika programu ya kurejea shule baada ya kupata changamoto mbalimbali za kimaisha ikiwamo ujauzito. Katika kituo hicho kuna jumla ya wanafunzi 50, kati…
Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan, atakuwa mwenyekiti mwenza katika mkutano wa nishati safi ya kupikia kwa Afrika utakaofanyika nchini Ufaransa. Anatarajiwa kuondoka nchini kesho Mei 12, 2024 kuhudhuria mkutano huo utakaofanyika Paris, Ufaransa. Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,…
MABIBGWA wa michezo ya kubashiri kampuni yaMeridianbet imefika kigamboni leo siku ya kina Mama duniani na kufanikiwa kutoa msaada katika Zahanati inayopatikana Mji mwema. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). Meridianbet wamekua na utaratibu wa kurudisha kwenye jamii yake pale ambapo wanahitajika na ndio walichokifanya leo, Kwani wametoa msaada wa vitu mbalimbali kama unga, mafuta,…
Dodoma. Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania (Red Cross Society) kikiadhimisha miaka 62 tangu kilipoanzishwa, kimekumbuka ushiriki wake katika kuhudumia waathirika wa ajali za MV Bukoba na treni Dodoma. Red Cross iliyoanzishwa nchini mwaka 1963 ilishiriki kutoa huduma kwa waathirika wa ajali ya MV Bukoba mwaka 1996 na ya treni ya mwaka 2002. Zaidi ya wanachama…