
Vitengo vya habari viendeshwe kwa weledi
KLABU za michezo ni taasisi kama taasisi nyingine zenye malengo ya kufikia na wadau wa kutumikia. Zinaweza kuwa taasisi za hiari au za kibiashara kutegemea walivyoamua waendeshaji wake. Klabu yoyote ya michezo ingependa ikue katika kufikia wadau wake. Ulimwengu wa sasa hauruhusu taasisi kuwasha taa yake na kuifunika. Mawasiliano yamekuwa ni mahitaji muhimu kwa taasisi…