
Wafanyakazi 5 wamefariki, 49 bado hawajulikani walipo baada ya jengo kuporomoka Afrika Kusini
Vikosi vya uokoaji vilifanya kazi usiku kucha kutafuta makumi ya wafanyikazi wa ujenzi waliozikwa kwa zaidi ya saa 12 chini ya vifusi vya saruji baada ya jumba la orofa nyingi lililokuwa likijengwa kuporomoka katika mji wa pwani nchini Afrika Kusini. Mamlaka ilisema mapema Jumanne (Mei. 7) kwamba idadi ya waliofariki imeongezeka hadi watano, huku wafanyakazi…