
Rais Vladimir Putin ala kiapo cha awamu ya tano ya urais – DW – 07.05.2024
Kwenye shughuli ya uapisho, Rais Vladimir Putinamesema anayachukulia mamlaka ya urais nchini humo kama “jukumu takatifu”. Akasisitiza katika Ukumbi wa Saint Andrew ambako amekula kiapo kwamba kuitumikia Urusi ni heshima kubwa, wajibu na jukumu takatifu, huku akiwarai raia wa taifa hilo kuvikabili vikwazo dhidi yao kwa kuungana pamoja. “Nina imani kuwa tutapita katika kipindi hiki…