
TANROADS RUVUMA YAFANYA UKARABATI MKUBWA WA MIUNDOMBINU KATIKA DARAJA LA MUHUWESI WILAYANI TUNDURU
Na Mwandishi Maalum Ruvuma WAKALA wa barabara Tanzania(TANROADS)Mkoa wa Ruvuma,imekamilisha kazi ya kuimarisha daraja la mto Muhuwesi wilayani Tunduru ambalo liliathirika na mvua za masika na kusababisha taaruki kwa watumiaji wa daraja hilo. Meneja wa TANROADS Mkoa wa Ruvuma Saleh Juma alisema,kwa sasa daraja hilo ni salama na haliwezi kusogea tena kama ilivyotokea hapo awali,…