
Guede alivyopindua meza ya usajili Yanga
MABAO manane yametosha kubadili sehemu ya usajili wa Yanga baada ya mabosi wa timu hiyo kushtuka kwamba mshambuliaji Joseph Guede ana kitu miguuni na kichwani, na sasa ni miongoni mwa mastaa wanaobaki Jangwani. Awali, Guede alionekana kuwa na mwanzo mgumu katika kikosi cha kocha Miguel Gamondi, lakini kadri muda unavyokwenda ameonekana kubadili upepo wa mambo…