
SERIKALI KUANZA UJENZI WA DARAJA LA MTO ATHUMANI
Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya amesema Serikali ipo katika hatua za mwanzo za maandalizi ya ujenzi wa daraja la mto Athumani lililopo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha. Akijibu swali bungeni leo, Mhe. Kasekenya amesema katika bajeti ya mwaka wa fedha 2024/25, Serikali imepanga kujenga na kukamilisha daraja hilo ili kunusuru maisha ya wananchi wa…