Mpina ‘anavyobanana’ na CCM | Mwananchi

Bariadi. Kauli ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Shemsa Mohammed ya kumtaka Mbunge wa Kisesa Wilaya ya Meatu mkoani humo, Luhaga Mpina kuacha siasa alizoziita za ‘majitaka’ imeendelea kukoleza msuguano kati ya mbunge huyo na chama chake. Mpina amekuwa kwenye msuguano na uongozi wa chama hicho mkoani Simiyu, kiasi cha kuitwa kwenye Kamati ya…

Read More

Kurugenzi waikimbia Moro Kids ‘playoff’ First League

Morogoro. Mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya mtoano (play off) baina ya Moro Kids ya Morogoro na Kurugenzi FC ya Simiyu umeshindwa kufanyika baada ya Kurugenzi kushindwa kufika katika mchezo uliopangwa kuchezwa leo, Aprili 27 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Mchezo huo maalumu wa kutafuta timu itakayocheza First League maarufu Ligi Daraja…

Read More

Msajili wa Hazina akutana na Bosi mpya wa Bodi ya Mikopo

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu, amekutana na kuzungumza na Menejimenti ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) iliyoongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wake Dk. Bill Kiwia. Kikao hicho kilifanyika katika Ofisi za Msajili wa Hazina Aprili 25, 2024 jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kujitambulisha kwa…

Read More

Waokota chupa za plastiki wakatiwa bima ya afya

Dar es Salaam. Wazalishaji wa vinywaji na watengenezaji wa bidhaa za plastiki nchini, wamewapatia waokota chupa za plastiki bima ya afya ya jamii (CHF) na viakisi mwanga vyenye namba kutokana na kuwa na mazingira hatarishi ya ufanyaji kazi zao. Katika kutambua mchango wa waokota chupa   hao wazalishaji wa  vinywaji nchini kwa kushirikiana na taasisi zinazojihusisha…

Read More

ALAT yawanyooshea kidole wabunge kwakutotetea maslahi ya madiwani

*Yataka uchaguzi wa madiwani utenganishwe ili wabunge waone ilivyo ngumu kupata kura Na Safina Sarwatt, Zanzibar BAADHI ya Wajumbe wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) wamewatupia lawama wabunge kwa kile kilichodaiwa kushindwa kuwatetea madiwani kuongezewa posho kutokana na mazingira magumu ya kazi na kupanda kwa gharama za maisha. Wajumbe hao wametaka kufabyika marekebisho…

Read More

Hizi ndizo tabia za Diarra, Aucho kambini Yanga

Kikosi cha Yanga jioni ya jana kilikuwa uwanjani kumalizana na Coastal Union katika mechi ya Ligi Kuu Bara, huku mastaa wa timu hiyo, Djigui Diarra, Maxi Nzengeli na Stephane Aziz KI walitarajiwa kuendeleza moto ulioifanya timu hiyo iwe tishio kwa sasa mbele ya wapinzani wanaochuana nao kuwania ubingwa. Hata hivyo, sasa unaambiwa tofauti na unavyowaona…

Read More

Mwanahabari Kabendera aituhumu Vodacom kufanikisha ‘kutekwa’ kwake

Dar es Salaam. Mwanahabari Erick Kabendera ameibua tuhuma nzito dhidi ya kampuni ya huduma za mawasiliano ya simu za mkononi, Vodacom, akiituhumu kuwa ndio iliyofanikisha kukamatwa kwake na askari Polisi, tukio analoliita kutekwa, na kisha kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi, mwaka 2019. Kutokana na madai hayo, Kabendera ambaye alikuwa amejikita katika uandishi wa habari za uchunguzi,…

Read More

China yatoa fursa zaidi Watanzania kujifunza Kichina

Dar es Salaam. China imetoa fursa ya Watanzania nchini  kupata ufadhili wa kusomeshwa katika Taifa hilo la pili kiuchumi na kwa idadi ya watu duniani. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam inayofundisha lugha ya Kichina (CI), Profesa, Zhang Xiaozhen, wakati wa kukabidhi msaada wa vitabu 100…

Read More