
Azam yaifuata Simba fainali Muungano
USHINDI wa mabao 5-2 ilioupata Azam FC dhidi ya KMKM, umeifanya timu hiyo kufuzu fainali ya Kombe la Muungano, michuano inayofanyika kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar. Azam imepata ushindi huo kupitia mabao ya Abdul Sopu dakika ya 7 na 42, huku wafungaji wengine wakiwa ni Nathaniel Chilambo (dk 9), Iddy Seleman (dk 49)…