
Mvua zasababisha vifo 155, Majaliwa atoa maelekezo 14
Dar es Salaam. Mvua kubwa za El-Nino zilizoambatana na upepo mkali, mafuriko na maporomoko ya udongo katika maeneo mbalimbali nchini zimesababisha vifo vya watu 155 na wengine 236 kujeruhiwa. Hayo yameelezwa bungeni leo Aprili 25, 2024 katika taarifa ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kuhusu changamoto za…