Msisitizo watolewa mashuleni kwa wanafunzi na wazazi

Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wamesisitizwa kuwa na nidhamu shuleni, kuzingatia masomo ili waweze kufanya vizuri kitaluma,kufaulu na kutimiza ndoto zao. Msisitizo huo umetolewa na Katibu Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Mungu Tanzania REV-Dismus Mofulu alipokuwa akizungumza katika Maafali Ya Kidato Cha Sita Katika Shule ya Sekondari ALDERZGETI iliyopo Babati Mkoani Manyara Amesema…

Read More

Tanzania nafasi ya 3 kwa tembo wengi barani Afrika

Imeelezwa kuwa Tanzania inaongoza kwa idadi kubwa ya simba, nyati, na chui huku ikishika nafasi ya tatu kwa kuwa na tembo wengi barani Afrika hivyo itachochea ongezeko la watalii na kufikia malengo ya serikali ya kufikisha idadi ya watalii milioni tano ifikapo 2025. Takwimu hizo zimetolewa na mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa wanyamapori Tanzania…

Read More

IMF NA EAC WAJADILI UKUSANYAJI MAPATO YA NDANI KWA AJILI YA MAENDELEO

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akizungumza katika mkutano uliotishwa na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF na kuwakutanisha Wadau kutoka nchi za Afrika Mashariki, wakati wa mikutano ya Kipupwe (Spring Meetings), jijini Washington D.C nchini Marekani, ambapo walijadili namna nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zinavyoweza kujitegemea kwa kuboresha na…

Read More

WAZIRI MAVUNDE  ASIKILIZA CHANGAMOTO ZA WADAU WA MADINI NCHINI

Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde leo Aprili 22, 2024 jijini Dodoma amekutana na wafanyabiashara wa madini na wachimbaji wa madini kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili kwenye shughuli zao ikiwemo changamoto ya ukosekanaji wa teknolojia ya uchenjuaji wa baadhi ya madini na hivyo kuielekeza Tume kuandaa utaratibu sahihi wa usafirishaji wa madini yaliyongezwa thamani…

Read More

WANAFUNZI KATIKA SHULE ZILIKUMBWA NA MAFURIKO WATAENDELEA NA MASOMO – WAZIRI MKENDA

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema Serikali imejipanga na itahakikisha wanafunzi ambao shule zao zimefungwa kutokana na mafuriko Nchini kote wanaendelea na masomo. Mkenda amebainisha hayo April 22, 2024 wakati akizungumza na wahanga wa mafuriko katika kijiji cha Muhoro na Chumbi B Wilayani Rufiji mkoani Pwani, ambapo amewasisitiza Wazazi kuwaruhusu Watoto…

Read More

MSAADA WA KIBINADAMU KWA WAHANGA WA MAFURIKO PWANI

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge (wa pili kulia) akipokea msaada wa kibinadamu kwa ajili ya wahanga wa mafuriko ya Rufiji na Kibiti wenye thamani ya takribani shilingi 250m uliotolewa na Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation. Msaada huo ulikabidhiwa na Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Vyombo vya Habari wa kampuni ya Vodacom Tanzania…

Read More