
Simba ilirahisisha ushindi wa Yanga Dabi
Ushindi wa mabao 2-1 ambao Yanga iliupata dhidi ya Simba katika dabi ya Kariakoo, Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, yanaweza kuwa matokeo yaliyorahisishwa kwa kiasi kikubwa na timu iliyopoteza mchezo huo. Hakikuwa kibarua kigumu kwa Yanga kupata ushindi katika mechi hiyo tofauti na uhalisia unaotakiwa wa timu kupaswa kufanya kazi ngumu kupata ushindi…