
Dk Nchimbi aibeba falsafa ya maridhiano ya Rais Samia
Songea. Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi amesema siasa ya vyama vingi si ugomvi, akiwataka wana-CCM na Watanzania kutoacha kuzungumza na kusalimiana, ili kujenga mshikamano wa Taifa. Amewataka wanachama wa CCM kuishi katika misingi ya kutogombana, ili kutunza dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhimiza maridhiano na umoja wa kitaifa…