
Mkuu wa Magereza acharuka wafungwa kufia gerezani
Morogoro. Kamishna Jerenali wa Magereza Tanzania, Mzee Nyamka amewataka watumishi wa jeshi hilo kutimiza wajibu wao kwa kuzingatia sheria na waache kujihusisha na matendo yanayolitia doa jeshi hilo, ikiwamo kuwapiga wafungwa ambao baadhi yao wameshapoteza maisha. Akizungumza leo Jumapili Aprili 20, 2024 mjini Morogoro wakati akifunga mafunzo ya uongozi daraja la kwanza ngazi ya sajenti…