
Makete mpya isiyo na vilio vya misiba tena
Njombe, Makete. Takriban miongo miwili iliyopita ilikuwa ni jambo la kawaida kuzika watu watatu mpaka wanne kwa siku waliofariki kutokana na maambukizi ya virusi vya Ukimwi (VVU) wilayani Makete. Wilaya hiyo ni miongoni mwa zilizoathiriwa zaidi na maambukizi VVU nchini na kupitia wakati usioelezeka, hasa ilipofikia hatua ya viongozi wa kaya (baba na mama) kufariki…