Kina Sanga wa Chadema waachiliwa huru kesi ya mauaji

Njombe. Mahakama Kuu Kanda ya Iringa imewaachia huru wanachama watatu wa Chadema akiwamo aliyekuwa Katibu wa Jimbo la Njombe, George Sanga na wenzake wawili waliokuwa wakituhumiwa kwa mauaji ya kada wa CCM, Emmanuel Mlelwa. Wengine walioachiliwa huru ni Gooddluck Mfuse na Octatus Mkwela, baada ya Mahakama hiyo kuona hawana hatia. Katika kesi iliyoendeshwa tangu mwaka…

Read More

Chalamanda na hesabu kali Mapinduzi Cup akiiwazia Kagera

KIPA wa Kagera Sugar ambaye amejumuishwa kwenye kikosi cha Kilimanjaro Stars kwa ajili ya michuano ya Kombe la Mapinduzi, Ramadhan Chalamanda amesema ataitumia kama daraja kujihakikishia namba katika mashindano mengine. Pia amesema wakati akijiandaa kisaikolojia kukabiliana na michuano hiyo kwa mara ya kwanza kwake, akili nyingine ipo Ligi Kuu namna ya kuipambania timu yake na…

Read More

Mapinduzi yalivyomkimbiza Sultan Jamshid | Mwananchi

Dar es Salaam. Wakati Wazanzibari wakikaribia kuadhimisha miaka 61 ya Mapinduzi, historia inamkumbuka sultani wa mwisho wa visiwa hivyo, Sayyid Jamshid bin Abdullah Al Said aliyefariki dunia jana nchini Oman akiwa na umri wa miaka 95. Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali vya kimataifa zimesema kuwa Sultan Jamshid alifariki jioni ya Desemba 30, 2024 katika Hospitali ya…

Read More

MHE. NDERIANANGA AKABIDHI MISAADA WAATHIRIKA MAFURIKO SAME

Na Mwandishi wetu- Kilimanjaro Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro kutenga bajeti kwa ajili ya kukabiliana na maafa yanapotokea pamoja kutambua maeneo hatarishi. Mhe. Nderiananga alitoa kauli hiyo wakati akikabidhi misaada ikiwemo mahindi tani 3.2, ndoo 25,…

Read More

2025 ni mwaka wa uchaguzi Afrika

Dar es Salaam. Wakati ulimwengu ukiupokea mwaka mpya 2025, mataifa 10 ya Afrika, ikiwemo Tanzania, yanatarajia kufanya uchaguzi mkuu mwaka huu kuchagua viongozi watakayoyaongoza kwa mujibu wa katiba zao. Mwaka 2024, mataifa 19 ya Afrika yalifanya uchaguzi mkuu ambapo imeshuhudiwa wagombea wa upinzani wakifanya vizuri kwenye chaguzi zilizofanyika kwenye mataifa kadhaa yakiwamo Senegal, Mauritius na…

Read More

Ligi Kuu Bara yasimama hadi Machi mosi, 2025

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania imetangaza kuwa baada ya michezo iliyofanyika Desemba 29, 2024 ligi hiyo itasimama hadi Machi mosi itakaporejea kwa mzunguko wa 17. Bodi ya Ligi imetaja sababu ya kusimama kwa Ligi ni kupisha mashindano ya Mapinduzi Cup yatakayo anza Januari 3 visiwani Pemba na mashindano ya fainali za mataifa ya Afrika CHAN…

Read More

Familia inavyomkumbuka Jaji Werema | Mwananchi

Dar es Salaam. Familia ya aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) mstaafu, Jaji Frederick Werema imesema kifo chake kimeacha simanzi na pengo, likiwamo la ushauri. Jaji Werema alifariki dunia jana Desemba 30, 2024 akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Akizungumza na Mwananchi leo Desemba 31, nyumbani kwa marehemu Mikocheni A, jijini Dar es…

Read More