
PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO DISEMBA 31, 2024
Home » PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO DISEMBA 31, 2024 About the author
Home » PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO DISEMBA 31, 2024 About the author
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya CRDB,Bw. Stephen Adili,akimkabidhi funguo za gari pamoja na vifaa mbalimbali Bw.Khamis Majala mara baada ya kuibuka mshindi katika kampeni yao ya Benki ni Simbanking hafla liyofanyika leo Disemba 30,2024 jijini Dodoma. Na.Alex Sonna-DODOMA Benki ya CRDB imemkabidhi gari jipya Bw.Khamis Majala baada ya kuibuka mshindi katika…
Na Mwandishi wetu Dodoma Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imewahimiza wananchi kutumia msimu wa sikukuu na likizo kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini ili kujifunza, kuburudika, na kuchangia ukuaji wa uchumi wa taifa. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma jana, Mkurugenzi wa Masoko wa TTB, Ernest Mwamwaja, alisema Tanzania imejaliwa kuwa na vivutio vya…
WIKI mpya imeanza ndani ya Meridianbet kwani leo hii unaweza ukajipigia mkwanja wako wa maana ukiweka dau lako dogo tuu. Timu kibao zipo uwanjani leo. Ingia na ubashiri sasa. EPL leo hii Aston Villa atakuwa pale nyumbani Villa Park kukiwasha dhidi ya Brighton ambao wametoka kutoa sare mechi yao iliyopita. Unai Emery na vijana wake…
SERIKALI imewahimiza wananchi kutumia msimu wa sikukuu na likizo kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini ili kujifunza, kuburudika na kuchangia ukuaji wa uchumi wa Taifa. Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana, Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Ernest Mwamwaja alisema Tanzania imejaliwa kuwa na vivutio vya kipekee ambavyo vinapaswa kuthaminiwa…
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar. Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, amesema chama hicho kimeendelea kutafsiri kwa vitendo sera zake za uimarishaji wa huduma za afya nchini zinazoendana na mahitaji ya wananchi wa makundi yote. Hayo ameyasema katika ziara yake ya kuwatembelea wagonjwa na watu wenye mahitaji maalum katika maeneo mbalimbali ya…
Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Eliakim Maswi amemtaja Mwanasheria Mkuu (AG) mstaafu, Jaji Frederick Werema kuwa mmoja wa viongozi waliokuwa na misimamo huku akikumbusha weledi aliouonyesha wakati wa sakata la akaunti ya Escrow. Kauli ya Maswi inakuja saa chache baada ya taarifa ya kifo cha Jaji Werema kilichotokea katika…
Unguja. Wakati Watanzania leo wakiuaga mwaka 2024 na kuukaribisha mwaka 2025, Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amewataka wananchi kuendelea kudumisha amani na mshikamano. Amesema mwaka 2025 ni wa uchaguzi mkuu, hivyo ni wajibu wa viongozi wa kisiasa, taasisi za kijamii, viongozi wa dini na wananchi wote kukumbushana umuhimu wa kudumisha na kuilinda amani ya…
Chunya. Waziri wa Madini, Athony Mavunde amesitisha shughuli ya uchimbaji madini ya dhahabu ndani ya Mto Zira uliopo katika Kijiji cha Ifumbo, Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya. Hatua hiyo imekuja siku chache baada kuibuka mgogoro wa wananchi na mwekezaji wa kampuni ya G&I Tech Traditional Company Limited, kulalamikia uharibifu wa mazingira na uchafuzi wa maji…
Mbeya. Wanafunzi wa vyuo vikuu na vya kati mkoani Mbeya wameunda Umoja wa Jamii ya Masai (Memasa), wenye lengo la kupinga mila potofu na kuhamasisha elimu katika jamii hiyo. Wakizungumza na Mwananchi leo Jumatatu, Desemba 30, 2024, wanafunzi hao wamesema umoja huo utakuwa suluhisho kwa changamoto zinazokwamisha haki ya elimu kwa vijana wa jamii hiyo,…