
CCM kurudisha serikalini mashamba ya ngano Hanang
Katesh /Liwale. Mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan, ameahidi kuimarisha kilimo cha ngano wilayani Hanang ili kufikia lengo la uzalishaji wa tani milioni moja ifikapo mwaka 2030. Amesema hilo litafanyika kwa kuyarudisha serikalini mashamba yaliyotolewa kwa wawekezaji lakini wakashindwa kuyaendeleza. Akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni leo Oktoba 3, 2025 katika…