
PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO JANUARI 5,2025
Home ยป PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO JANUARI 5,2025 About the author
Home ยป PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO JANUARI 5,2025 About the author
Mkutano wa Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umefanyika Zanzibar tarehe 04 Januari, 2025 chini ya uenyekiti wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thatib Kombo akishirikiana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Stergomena…
Na Issa Mwdangala Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Augustino Ignace Senga amefanya baraza na askari wa Mkoa wa Songwe Januari 03, 2025 katika ukumbi wa Polisi uliyopo Vwawa Wilaya ya Mbozi na kuwataka askari hao kuendelea kutekeleza jukumu mama la kulinda raia na mali zao ikiwa ni pamoja…
Same. Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amewataka wataalamu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) wanaojenga Daraja la Mpirani wilayani Same kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha linakamilika ndani ya siku tatu. Daraja hilo lililopo Kijiji cha Mpirani, Kata ya Maore, lilivunjika Januari 2, 2025 baada ya nguzo kuathiriwa na maji ya mvua. Kuvunjika kwa daraja…
NA DENIS MLOWE, IRINGA Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Daudi Yassin, amesema kuwa ushindi mkubwa walioupata katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji, na vitongoji imetokana na utekelezaji wa ilani ya chama hicho chini ya Rais Samia Suluhu Hassan na kuwashukuru wananchi kwa kuwapigia kura. Yasin alisema hayo wakati akizungumza na…
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chauma), Hashim Rungwe amewashauri wagombea wa nafasi mbalimbali ndani ya Chadema, kuepuka kupigana madongo badala yake waeleze nini watakachokifanya ili wajumbe wawachague. Chadema inatarajia kufanya uchaguzi mkuu ifikapo Januari 21, 2025, ambapo wajumbe watachagua viongozi wa kitaifa, ukitanguliwa na chaguzi za mabaraza ya chama hicho….
Na Issa Mwadangala Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Augustino Ignace Senga ametoa Zawadi kwa askari waliofanya vizuri katika kazi za Polisi baada ya kukagua mazoezi yaliyoandaliwa na Kikosi cha kutuliza Ghasia Mkoa wa Songwe. Zawadi hizo ni pamoja na pesa taslimu zilizotolewa Januari 04, 2025 na kueleza kuwa…
Tanga. Wanachama wa Umoja wa Wamiliki wa Waendesha Pikipiki na Bajaji Wilaya ya Tanga (Uwapibata) wamechanga Sh1 milioni kwa ajili ya Rais Samia Suluhu Hassan kuchukua fomu ya kugombea urais kwa mwaka 2025. Fedha hizo wamezikabidhi leo Januari 4, 2025, wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Tanga, Ummy Mwalimu, jijini hapa….
WADAU Wa Sekta ya Urembo na Mitindo wameihimiza serikali kuweka Mazingira bora ya uwakala wa bidhaa za kimataifa za vipodozi ili kupunguza changamoto ya bidhaa bandia zinazosambazwa nchini. Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa tawi jipya la Duka la Dawa baridi na Vipodozi Mkurugenzi wa CAICA Pharmacy, Jackson John, amesema Kampuni yake inalenga kuwa mfano…
Same. Changamoto ya usafiri na usafirishaji katika Tarafa za Mamba Myamba na Gonja wilayani Same, Mkoa wa Kilimanjaro, inaelekea kuwa historia baada ya Serikali kuanza ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilomita 36 kutoka Ndungu hadi Mkomazi. Wakati mkandarasi akikabidhiwa jukumu la ujenzi wa barabara hiyo, pia Serikali imekamilisha mchakato wa kumpata mkandarasi atakayejenga takribani…