Matumaini wawekezaji kutoka Japan wakitua Tanzania

Dar es Salaam. Kampuni 20 za uwekezaji kutoka nchini Japan zimekuja Tanzania kuangalia fursa za uwekezaji katika maeneo ya kilimo, utalii na sekta ya uzalishaji viwandani ikiwa ni sehemu ya kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili. Kampuni hizo zimekutana na nyingine 50 za Kitanzania kwa lengo la kubadilishana uzoefu, teknolojia sambamba na kufanya biashara…

Read More

Wazazi wakumbushwa kutimiza wajibu wa malezi

Njombe. Kamati ya Shule ya Msingi NjooMlole iliyopo Halmashauri ya Mji wa Njombe imewataka wazazi kutimiza wajibu wao wa malezi kwa kuhakikisha wanawanunulia watoto wao vifaa vinavyohitajika shuleni ikiwamo sare za shule, madaftari na kupeleka vyakula shuleni ili wasome kwa uhuru na kufaulu masomo yao. Hayo yamesemwa leo Januari 14, 2025 na Mwenyekiti wa Kamati…

Read More

Rais Samia ahutubia Mabalozi pamoja na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa katika Sherehe za Mwaka Mpya kwa Mabalozi (Diplomatic Sherry Party) Ikulu Jijini Dar

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye Sherehe za Mwaka Mpya kwa Mabalozi (Diplomatic Sherry Party) Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Januari, 2025.      Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania pamoja na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa wakiwa kwenye Sherehe za Mwaka Mpya kwa Mabalozi hao (Diplomatic…

Read More

Madereva walia na maegesho ya magari Kendwa

Unguja. Madereva wa magari ya utalii Kijiji cha Kendwa, Mkoa wa Kaskazini Unguja wameiomba Serikali kuwapatia eneo la maegesho ya magari ili kuondokana na usumbufu unajitokeza. Wamezungumza hayo katika kikao cha Katibu Tawala Wilaya ya Kaskazini A, Unguja, leo Januari 14, 2025, kilichowakutanisha madereva hao kuzungumzia changamoto mbalimbali. Dereva Abdulla Abdi Ahmada amesema awali walikuwa…

Read More

Simulizi ajali iliyoua 11 wakiokoa majeruhi

Dar/Tanga. Ni siku zisizozidi 20 zikichukua maisha ya watu 30 kutokana na ajali za barabarani zilizotokea kati ya Desemba 24, 2024 na Januari 13, 2025, wilayani Handeni Mkoa wa Tanga. Ajali tatu zilizotokea wilayani humo pia zimesababisha majeruhi zaidi ya 35. Katika tukio la hivi karibuni, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi amesema…

Read More

Wajasiriamali waeleza walivyonufaika na Tasaf

Unguja. Wajasiriamali waliopo kwenye mpango wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) wameeleza namna ulivyowaondoa kwenye umaskini. Mpango wa kunusu kaya maskini kwa Zanzibar ulianza mwaka 2013 ukiwa katika afua tatu za ruzuku, ajira za muda na miundombinu. Mpaka sasa kuna vikundi 3,372 vyenye wanachama 45,948. Vikundi hivyo vimekusanya akiba ya zaidi ya Sh1.6 bilioni…

Read More