
Jela miaka 15 kwa kumuua mkewe bila kukusudia
Geita. Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Geita imemhukumu kifungo cha miaka 15 jela, Andrea George (21) kwa kosa la kumuua mkewe, Tabu Jems bila kukusudia. Hukumu hiyo imetolewa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Kelvin Mhina baada ya kusikiliza kesi hiyo iliyokuja mahakamani hapo leo Januari 20,2025 kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa maelezo ya awali…