
Mahitaji ya vifaa vya viwandani yaongezeka nchini
Dar es Salaam. Ripoti ya uagizaji wa bidhaa kutoka nje kwa mwaka 2024 inaonyesha uagizaji mkubwa wa vifaa vya viwandani, hali inayoakisi ukuaji wa sekta ya viwanda nchini. Takwimu zinaonyesha kuwa jumla ya Sh43.076 trilioni zilitumika kuagiza bidhaa mbalimbali, huku vifaa vya viwandani vikiongoza kwa thamani ya Sh11 trilioni, ikifuatiwa na chuma na bidhaa zake…