
Waziri Ulega aitaka Tanroads kuweka taa za barabarani Dakawa
Morogoro. Waziri wa Ujenzi, Abdalah Ulega, amemuagiza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Dk Charles Msonde, kuhakikisha eneo la Dakawa, lililopo wilayani Mvomero, linawekwa taa za barabarani na kujengwa maeneo ya maegesho ya magari ili kuwezesha wananchi kufanya shughuli zao wakati wote. Ulega ametoa agizo hilo leo Jumatatu, Januari 13, 2025 wakati wa ziara…