
Vitambulisho 31,000 vya Nida vilivyofutika kutengenezwa upya
Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amesema alishatoa maagizo kwa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), kutengeneza upya vitambulisho takribani 31,000 vilivyofutika taarifa zake. Waziri huyo amesema amepokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusiana na ubora hafifu wa vitambulisho hivyo na kuagiza vitengenezwe upya. Waziri Bashungwa ametoa kauli hiyo…