Hii hapa ratiba nzima sherehe ya Mapinduzi Zanzibar
Unguja. Leo ikiwa ni kilele cha maadhimisho ya miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar, wananchi wameanza kuingia katika Uwanja wa Gombani, Wilaya ya Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba zinapofanyika sherehe hizo. Katika sherehe hizo ambazo wageni waalikwa na viongozi mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wanatarajiwa kuanza kuingia uwanjani hapo kuanzia saa 6:35 mchana,…