Polisi walivyodhibiti majambazi waliovaa magauni, vilemba Mwanza
Mwanza. Wanaume wawili wanaosadikiwa kuwa majambazi wenye silaha wameuawa kwa kupigwa risasi na askari wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, baada ya kudaiwa kujaribu kutekeleza tukio la ujambazi. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbrod Mutafungwa akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Januari 10, 2025 amesema wanaume hao ambao walivaa magauni na vilemba kuficha…