Watu sita kortini wakidaiwa kutumia EFD kuhujumu uchumi
Dar es Salaam. Watu sita wakiwamo wafanyabiashara wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni iliyoko Kinondoni, wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa kutumia mashine ya kielektroniki ya kutolea risiti (EFD). Washtakiwa hao ni Stanslaus Mushi, Edwin Mark na Nemence Mushi ambao ni wafanyabiashara, Rose Nanga (mhasibu), Hussein Mlezi, (fundi kompyuta) na Salim Kajiru…