Simba yaongeza Straika | Mwanaspoti
BAADA ya Simba Queens kumtambulisha golikipa, Wilfrida Seda kutoka Get Program, timu hiyo imemvuta tena straika Janet Mpeni kutoka timu hiyo. Kama usajili huo utakamilika, Simba Queens hadi sasa itakuwa imefikisha nyota watatu, Seda, Mpeni na Zawadi Khamis kutoka Fountain Gate Princess ambaye hajatambulishwa kikosini hapo. Nyota huyo kwa sasa yuko kwenye majukumu ya timu…