
Mawasiliano Same bado baada ya daraja kukatika
Same. Mawasiliano ya barabara kuu ya Same-Mkomazi, wilayani Same, Mkoa wa Kilimanjaro yameendelea kukwama kwa siku ya pili, mamlaka husika zikiendelea kutafuta ufumbuzi. Mkwamo wa mawasiliano unatokana na Daraja la Mpirani kukatika jana Januari 2, 2025 saa mbili asubuhi kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Daraja hilo ndilo kiungo cha kata na makazi ya wananchi wanaoishi…