
January 2025


EXIM BANK YAENDELEA KUJIIMARISHA KWA UNUNUZI WA CANARA BANK TANZANIA
Benki ya Exim Tanzania inayo furaha kutangaza kukamilika kwa ununuzi wa Canara Bank Tanzania Limited. Huu ni ununuzi wa benki ya tatu ambao umefanyika na Benki ya Exim ndani ya miaka sita iliyopita, ikizidi kuimarisha nafasi yake kama mdau muhimu katika sekta ya benki nchini Tanzania. Ununuzi huu ulianza kwa kusainiwa kwa makubaliano mnamo mwaka…


Ndege nyingine yawaka moto Korea Kusini, watatu wajeruhiwa
Seoul. Majanga katika usafiri wa anga yameendelea kuikumba Korea Kusini baada ya ndege ya Shirika la Busan nchini humo kushika moto muda mfupi kabla ya kuanza safari yake kwenda Hong Kong. Shirika la Habari la Associated Press (AP) limeripoti kuwa ndege hiyo imeshika moto saa 4:30 usiku wa kuamkia leo, Jumatano, Januari 29, 2025, katika…

Chadema kuendesha siasa za shuruti kuelekea uchaguzi mkuu
Dar es Salaam. Wakati viongozi wa wa juu wa Chadema wakipanga wiki moja ya kikao cha kupanga mikakati ya kuendesha chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu, Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu amesema chama hicho kitaendesha siasa za kushurutisha mageuzi ya kisiasa. Lissu amesema hayo leo Jumatano, Januari 29, 2025, alipofika ofisi za…

Serikali kukamilisha mwongozo wa watumishi wanaojitolea
Dodoma. Serikali imesema iko katika hatua za mwisho kukamilisha mwongozo utakaoangalia jinsi ya kuwaingiza katika mfumo watumishi wanaojitolea nchini. Akizungumza bungeni leo, Jumatano, Januari 29, 2025, Naibu Waziri katika Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deus Sangu alisema mwongozo huo utakuwa na mchakato wa kuwaingiza watumishi hao katika mfumo rasmi,…

Rais Samia ampongeza Padri Mihali kuteuliwa Askofu wa Jimbo la Iringa
Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amempongeza Padri Romanus Elamu Mihali kwa kuteuliwa na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Fransisko, kuwa Askofu mteule wa Jimbo Katoliki la Iringa. Padri Mihali aliteuliwa jana Jumanne, Januari 28, 2025, kuchukua nafasi ya Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa, baada ya kuridhia ombi lake la kustaafu. Leo Jumatano,…

Mjue Mwanamke Mrefu na Mfupi Duniani, Washangaza – Video – Global Publishers
Wanawake wawili waliovunja rekodi za dunia kwa urefu na ufupi wao hivi karibuni walikutana kwa mara ya kwanza jijini London, Uingereza, na kutumia nafasi hiyo kuwahamasisha watu kote ulimwenguni kusherehekea tofauti zao za kimaumbile. Rumeysa Gelgi, mwanamke mrefu kuliko wote duniani mwenye umri wa miaka 27, ni mtaalam wa masuala ya tovuti…

Mbunge ataka sheria ya kuwahasi wabakaji watoto
Dodoma. Kwa mara nyingine suala la ubakaji bungeni, safari hii mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Asya Sharif Omar, amehoji ni lini Serikali itapeleka seria ya kuwahasi wabakaji wanaofanya udhalilishaji wa kijinsia kwa watoto. Takwimu za Msingi Tanzania zilizotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), zinaonyesha kuwa matukio ya ubakaji yameongezeka kutoka 8,691 mwaka 2022…

Tundu Lissu Azungumza Maneno Mazito, Amvaa Wasira, Chalamila – Video – Global Publishers
Mwenyekiti Mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu leo amekabidhiwa ofisi rasmi na Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika kwenye ofisi za chama hicho, Mikocheni jijini Dar es Salaam. Lissu alishinda nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu uliofanyika Januari 21, 2025 ambapo alikuwa akichuana na Freeman Mbowe. …