
KONA YA MALOTO: Mtihani wa Lissu Chadema ni sawa na Ruto Kenya
Uchaguzi unapoisha, macho yote humtazama aliyeshinda. Matarajio huwa mengi endapo mshindi anakuwa mpya kwenye kiti. Mategemeo huwa na nguvu zaidi pale mshindi mpya anapofanikiwa kupitia agenda ya kumsiliba mtangulizi wake. Ilitokea Kenya kama mfano dhahiri. Rais William Ruto, hadi sasa bado anateswa na urais wake. Tangu alipokula kiapo kuiongoza nchi hiyo, Septemba 13, 2022, amekuwa…